HAKIKA BURIANI BABA YETU, ASKOFU MKUU!!
KAZI YA MUNGU INAENDELEA KWA WATUMISHI WAKE WALIO HAI. ASKOFU NA MCHUNGAJI WA KANISA HILI (EAGT KIMARA JESUS MIRACLE CENTRE) DR WILLY MATINGISA, BAADA YA KUKATISHA ZIARA YA MIKUTANO YA NJE YA NENO LA MUNGU, KUTOKANA NA MSIBA MKUBWA WA KITAIFA WA ASKOFU MKUU WA EAGT, DR MOSES KULOLA, SASA MKUTANO HUO UNAENDELEA KATIKA KIJIJI CHA CHALI MKOANI DODOMA.
IKUMBUKWE KABLA YA MSIBA, ZIARA YA MIKUTANO ILIANZIA KIJIJI CHA MTERA, MPAKANI MWA MIKOA YA IRINGA NA DODOMA.
MKUTANO WA INJILI KIJIJINI CHALI UMEANZA LEO TEREHE 10/09/2013 KATIKA VIWANJA VYA KIJIJI HICHO. MKUTANO UTAMALIZIKA TEREHE 15/09/2013.
KATIKA MKUTANO HUO WA INJILI KIJIJINI CHALI, MAHALI AMBAPO HAKUNA DESTURI YA WAHUBIRI NA WAINJILISTI KUFIKA, MCHUNGAJI MATINGISA AMEONGOZANA NA MAMA MCHUNGAJI SOPHYMARRY MATINGISA, PAMOJA NA KUNDI ZIMA LA KWAYA KUU YA KANISA-GSS, WAKIWA WAMESAFIRI NA VYOMBO VYA INJILI NA GENERETA.
GHARAMA ZA MKUTANO HUU- usafiri wa kukodi, mafuta, chakula na maamdalizi mengineyo ZIMEBEBWA NA WASHIRIKA WA KANISA LA KIMARA EAGT JESUS MIRACLE CENTRE. HAKIKA MUNGU ATAWALIPA KWA KULIFIKISHA NENO LA MUNGU HUKO CHALI-DODOMA.
ASKOFU NA MCHUNGAJI DR WILLY MATINGISA ANATOA WITO WA BARAKA KWA WADAU MBALIMBALI NCHINI NA HATA NJE YA NCHI KUTUMIA FURSA HIZI ZA UENEZAJI WA INJILI VIJIJINI NA MAHALI PENGINE KATIKA UTOAJI WENYE BARAKA.
CHANGIA HUDUMA YA INJILI VIJIJINI CHINI YA KANISA HILI NA MTUMISHI WA MUNGU. HAKIKA UTABARIKIWA KAMA BIBLIA INAVYO AGIZA.
KWA MCHANGO WAKO WA FEDHA AU KITU CHOCHOTE KIASI CHOCHOTE, TAFADHARI WASILIANA NA:
0754860070 AU 0715860070- MCHUNGAJI WILLY MATINGISA.