Taarifa ambazo zimetufikia leo zinasema kuwa Askofu Mkuu wa
Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia leo asubuhi. Hakika nio simanzi kubwa kwetu wana EAGT na watoto wote wa KIROHO wa enzi za utumishi wa huyu mzee!!
Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika ambazo BLOG hii ya EAGT KIMARA chini ya ASKOFU MATINGISA imezipata kutoka kwa watu wa ndani wa familia hiyo, zinaeleza kuwa Askofu Kulola amefariki katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam.
Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu.

Katika uhai wake, amepata watoto wengi wa kiroho ikiwemo Dr Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zakaria Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi.
BWANA ametoa na BWANA ametwaa, jina la BWANA lihimidiwe.
***
UPDATES (1700 hrs):
Msiba utakuwa kanisa la EAGT Temeke, na hapo shughuli nyingine zote zitafahamika hapo, mwili utatolewa AMI na kupelekwa Kairuki Hospital. Na pia watasafirisha mwili kuelekea MWANZA