Sunday, November 3, 2013

MKUTANO MKUBWA INJILI KUANZA EAGT KIMARA/TEBE CRUSADE AT EAGT KIMARA CHURCH

MCHUNGAJI DR. WILLY MATINGISA NA BARAZA LA WAZEE WA EAGT KIMARA, WANATANGAZA MKUTANO MKUBWA WA INJILI UTAKAO FANYWA NA KURUGENZI YA TEBE JIMBO LA KINONDONI.

  • MKUTANO HUU UTAANZA JUMATATU TAREHE  4 HADI 10 NOVEMBA.

  • MAHALI: ENEO LA UWANJA WA KANISA EAGT KIMARA.

  • MUDA: KUANZIA SAA 9 HADI SAA 12 JIONI.

  • WAHUBIRI: MHUBIRI CHINI YA TEBE JIMBO LA KINONDONI

  • UIMBAJI: KWAYA ZA KANISA LA EAGT KIMARA (GSS & GGC) NA WAALIKWA WENGI.
KARIBUNI WATU WOTE, MWAMBIE NA MWENZAKO. MKUTANO HUU SI WA KUKOSA KWAKUWA WATUMISHI WA MUNGU WAMEJIANDAA VEMA KIROHO, ILI MUNGU AWEZE KUKUHUDUMIA WEWE MWENYE SHIDA NA VIFUNGO VYA NAMNA ZOTE NA KUPEWA BARAKA UNAZOSTAHILI.

KUMBUKA "KWA YESU YOTE YANAWEZEKANA!!!!!!"

A BLESSING MOMENT!!!!!!

KINDLY A TEBE CRUSADE INVITATION MESSAGE FROM BISHOP, REV. DR MATINGISA & HIS ELDERS.
  • A CRUSADE TO BE CONDUCTED AT EAGT KIMARA CHURCH GROUNDS.
  • STARTS ON 4th to 10th NOVEMBER
  • EVERYDAY FROM 15 hours to 18 hours
  • EAGT KIMARA CHOIRS, SINGERS AND THE INVITED WILL MINISTER DURING THE CRUSADE.
  •  YOU ARE ALL INVITED AS MEN OF GOD HAVE SPIRITUALLY PREPARED TO DELIVER THE RESOURCEFUL MESSAGE FROM THE LIVING GOD.
  • FOR SURE THERE WILL BE HEALING AND BLESSINGS FROM GOD, DON'T PLAN TO MISS IT. 
WE ALSO ENCOURAGE EVERYONE OUT THERE TO BECOME PART OF THIS CRUSADE, AS GOD IS GOING TO MANIFEST HIS GLORIOUS POWER TO HIS PEOPLE. YOU WILL BE BLESSED UPON GIVING YOUR CONTRIBUTION (MONEY CONTRIBUTION TO FACILITATE THE CRUSADE). 

PLEASE FEEL BLESSED TO CONTACT Rev DR MATINGISA - 0754860070.

REMEMBER " EVERYTHING IS POSSIBLE TO GOD"

Monday, September 16, 2013

BISHOP DR MATINGISA AMALIZA MKUTANO WA INJILI KIJIJINI CHALI.

HAKIKA MUNGU NI MWEMA, MKUTANO WA INJILI KIJIJINI CHAALI CHINI YA MHUBIRI ASKOFU DR MATINGISA WAMALIZIKA KWA MAVUNO YA WATU WENGI KUOKOKA. ZILIKUWA NI SIKU 6 ZA MUNGU KUJITWALIA UTUKUFU NA KUWAPATA WALIO WAKE.

MHUBIRI NA WATUMISHI WENGINE WALIO AMBATANA NAYE HAKIKA WAMEFANYA MAJUKUMU YAO KAMA WATUMISHI WA MUNGU. KWA WALIOBAKI MUNGU ANAWAKUMBUKA KWA MAOMBI NA MALI ZAO.

Tuesday, September 10, 2013

R.I.P ASKOFU MKUU; ASKOFU WILLY MATINGISA, SAFARINI KIJIJI CHA CHALI, DODOMA KWA MKUTANO WA NJE.

HAKIKA BURIANI BABA YETU, ASKOFU MKUU!!

KAZI YA MUNGU INAENDELEA KWA WATUMISHI WAKE WALIO HAI. ASKOFU NA MCHUNGAJI WA KANISA HILI (EAGT KIMARA JESUS MIRACLE CENTRE) DR WILLY MATINGISA, BAADA YA KUKATISHA ZIARA YA MIKUTANO YA NJE YA NENO LA MUNGU, KUTOKANA NA MSIBA MKUBWA WA KITAIFA WA ASKOFU MKUU WA EAGT, DR MOSES KULOLA, SASA MKUTANO HUO UNAENDELEA KATIKA KIJIJI CHA CHALI MKOANI DODOMA.

IKUMBUKWE KABLA YA MSIBA, ZIARA YA MIKUTANO ILIANZIA KIJIJI CHA MTERA, MPAKANI MWA MIKOA YA IRINGA NA DODOMA.

MKUTANO WA INJILI KIJIJINI CHALI UMEANZA LEO TEREHE 10/09/2013 KATIKA VIWANJA VYA KIJIJI HICHO. MKUTANO UTAMALIZIKA TEREHE 15/09/2013.

KATIKA MKUTANO HUO WA INJILI KIJIJINI CHALI, MAHALI AMBAPO HAKUNA DESTURI YA WAHUBIRI NA WAINJILISTI KUFIKA, MCHUNGAJI MATINGISA AMEONGOZANA NA MAMA MCHUNGAJI SOPHYMARRY MATINGISA, PAMOJA NA KUNDI ZIMA LA KWAYA KUU YA KANISA-GSS, WAKIWA WAMESAFIRI NA VYOMBO VYA INJILI NA GENERETA.

GHARAMA ZA MKUTANO HUU- usafiri wa kukodi, mafuta, chakula na maamdalizi mengineyo ZIMEBEBWA NA WASHIRIKA WA KANISA LA KIMARA EAGT JESUS MIRACLE CENTRE. HAKIKA MUNGU ATAWALIPA KWA KULIFIKISHA NENO LA MUNGU HUKO CHALI-DODOMA.

ASKOFU NA MCHUNGAJI DR WILLY MATINGISA ANATOA WITO WA BARAKA KWA WADAU MBALIMBALI NCHINI NA HATA NJE YA NCHI KUTUMIA FURSA HIZI ZA UENEZAJI WA INJILI VIJIJINI NA MAHALI PENGINE KATIKA UTOAJI WENYE BARAKA.

CHANGIA HUDUMA YA INJILI VIJIJINI CHINI YA KANISA HILI NA MTUMISHI WA MUNGU. HAKIKA UTABARIKIWA KAMA BIBLIA INAVYO AGIZA.

KWA MCHANGO WAKO WA FEDHA AU KITU CHOCHOTE KIASI CHOCHOTE, TAFADHARI WASILIANA NA:

0754860070 AU 0715860070- MCHUNGAJI WILLY MATINGISA.

Thursday, August 29, 2013

NI SIMANZI KUBWA EAGT TAIFA- ARCH BISHOP MOSES KULOLA IS NO LONGER

Taarifa ambazo zimetufikia leo zinasema kuwa Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia leo asubuhi. Hakika nio simanzi kubwa kwetu wana EAGT na watoto wote wa KIROHO wa enzi za utumishi wa huyu mzee!!
Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika ambazo BLOG hii ya EAGT KIMARA chini ya ASKOFU MATINGISA imezipata kutoka kwa watu wa ndani wa familia hiyo, zinaeleza kuwa Askofu Kulola amefariki katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam.

Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu.


Katika uhai wake, amepata watoto wengi wa kiroho ikiwemo Dr Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zakaria Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi.



BWANA ametoa na BWANA ametwaa, jina la BWANA lihimidiwe.
***

UPDATES (1700 hrs):
Msiba utakuwa kanisa la EAGT Temeke, na hapo shughuli nyingine zote zitafahamika hapo, mwili utatolewa AMI na kupelekwa Kairuki Hospital. Na pia watasafirisha mwili kuelekea MWANZA

Tuesday, August 20, 2013

KARIBU KATIKA BLOG YA KANISA LA EAGT KIMARA


A WELCOME NOTE FROM THE PASTOR, REV. DR WILLY MATINGISA TOGETHER WITH HIS CHURCH ELDERS.

YOU ARE WARMLY WELCOME TO VISIT OUR BLOG ABOUT CHURCH SERVICES AND VARIOUS DEVELOPMENT PLANS.
WE ARE GRATEFUL TO ASK YOU TO SHARE WITH US GOOD NEWS ABOUT GOD'S WORK TO HIS PEOPLE; TO SHARE EXPERIENCES ON SERVING GOD AND TO HELP US ON VARIOUS DEVELOPMENT INITIATIVES.

GOD BLESS YOU AND LET US KNOW WHAT YOU THINK ABOUT OUR CHURCH. 
 
AGAIN YOU ARE WELCOME!

MCHUNGAJI DR. WILLY R. MATINGISA NA BARAZA LAKE LA WAZEE LINAWAKARIBISHA WATU WOTE KATIKA BLOG HII YA KANISA.

KANISA LIMETAMBUA UMUHIMU WA TEKNOLOJIA KATIKA MAWASILIANO NA UENEZAJI HABARI, NA HIVYO KWA KUPITIA BLOG HII, KANISA LITAJITANGAZA KWA WATU WOTE TANZANIA NA NJE YA TANZANIA.

KUPITIA BLOG HII MTAZAMAJI ATAWEZA KUJIONEA MAMBO MBALIMBALI MHIMU YANAYO ENDELEA KATIKA KANISA HILI.

WADAU; WASHIRIKA WA KANISA HILI NA WASIO WANAOMBWA KUSHIRIKI PROGRAMU MBALIMBALI ZA MAENDELEO YA KANISA HILI KATIKA NYANJA ZA KIROHO NA KIMAENDELEO YA UCHUMI NA KIJAMII.

KARIBU EAGT KIMARA NA MUNGU ATAKUBARIKI SANA!

MKUTANO MKUBWA JIJINI MWANZA KWA MARA NYINGINE

NI  MKUTANO MKUBWA WA NENO LA MUNGU ULIOAZA 11/11/2018 MWANZA ILEMELA MKUTANO HUO UNAHUBILIWA NA DR WILE MATINGISA WALETE WATU WENYE SHIDA M...